Msako Wa Makaa Kajiado

  • last year
Washikadau Katika Eneo La Lukung'u Bisil Kaunti Ya Kajiado Wameapa Kukabiliana Na Biashara Haramu Ya Kuuza Makaa Wakiitaja Kama Iliyochangia Hali Ya Tabianchi.Katika Msako Uliokuweko Huo Magunia Yapatayo Mia Moja Na Tatu Yalinaswa Huku Polisi Wakiendelea Kusaka Washukiwa Watatu Sugu.Katika Oparesheni Iliyokuwa Ikiongozwa Na Naibu Kaunti Kamishna Harun Kamau, Kamau Amedokeza Kwamba Hawatolegeza Mwendo Katika Harakati Ya Kukabiliana Na Suala Hilo.Kwa Upande Wake Mkurugenzi Wa Mazingira Nathan D. Kobaai Amedokeza Kwamba Kiangazi Upande Wa Kajiado Kimechangiwa Na Moja Wepo Ya Sababu Ikiwa Kuchoma Kwa Makaa. Aidha Wamewataka Wananchi Kuwa Macho Kukomesha Biashara Hii Na Kwamba Wataezeka Vizuizi Barabarani Hadi Wawakamate Washukiwa Wote.