Christian Video Swahili “Uaminifu ni wa Thamani Mno” | Wokovu wa Bwana

  • 6 years ago
Zhen Cheng alikuwa mmiliki wa duka la urekebishaji wa vifaa vya stima. Alikuwa mkarimu, mwaminifu, na alifanya biashara inavyopasa kufanywa. Hangejaribu kumdanganya mtu, lakini alikuwa anachuma tu pesa za kutosha angalau kuimudu tu famillia yake. Baada ya muda, mmoja wa jamaa yake na mfanya biashara mwenza alimhimiza atende kulingana na sheria zisizoandikwa za biashara, na Zhen Cheng alianza kuamini katika misemo inayowakilisha falsafa ya kama vile: “Mwanaume bila kipato cha pili hawezi kamwe kuwa tajiri kama tu jinsi farasi aliyenyimwa nyasi kavu usiku hawezi kamwe kuongeza uzani,” “Wajasiri hufa kwa ajili ya tamaa; waoga hufa kwa njaa,” “Pesa si kila kitu, lakini bila pesa, huwezi kufanya chochote,” na “Pesa kwanza.”
Zhen Cheng alipoteza dhamiri yake nzuri iliyokuwa imemwelekeza awali na akaanza kutumia mbinu za kisirisiri kupata pesa zaidi. ... Baada ya Zhen Chen kuikubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho, alikuja kuelewa kupitia neno la Mungu kwamba Mungu anawapenda watu waaminifu na Anawachukia walio wadanganyifu. Zhen Cheng pia alikuja kuelewa kwamba kuwa mtu mwaminifu ndiyo njia ya pekee ya kutenda kama mtu wa kweli na njia ya pekee ya kufanikisha sifa ya Mungu, na hivyo akaapa kuwa mtu mwaminifu. Hata hivyo, kuwa mtu mwaminifu katika maisha halisi kulidhihirika kuwa kugumu: Pamoja na ndugu kanisani, angeweza kuwa mnyoofu alivyopaswa kuwa, lakini angefanya hivyo katika ulimwengu wa biashara, angeweza kupata pesa? Hangeweza tu kwa matarajio ya kupata pesa chache zaidi, angeweza pia kupitia hasara kubwa na alikuwa katika hatari ya kupoteza duka lake. … Usoni pa mapambano kama hayo, je, Zhen Chen angeweza kuendesha biashara yake kwa uaminifu? Ni mabonde na milima ya aina gani yasiyotarajiwa yatatokea njiani? Thawabu yake kubwa itakuwa nini?…

Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.

Kauli Maalum: Uzalishaji huu wa video ulitengenezwa kama mradi usio wa faida na Kanisa la Mwenyezi Mungu. Wahusika wanaoonekana katika uzalishaji huu wanafanya kwa msingi wa kutotafuta faida, na hawajalipwa kwa njia yoyote. Video hii isisambazwe kwa mtu mwingine kwa minajili ya faida, na ni matumaini yetu kwamba kila mtu atashiriki kuigawa na kuisambaza hadharani. Wakati unapoisambaza, tafadhali sisitiza chanzo chake. Bila ridhaa ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, hakuna shirika, kundi la kijamii, au mtu binafsi anayeweza kubadilisha au kuhudhurisha visivyo maudhui ya video hii.

Baadhi ya vifaa ni kutoka:
https://www.youtube.com/watch?v=GNDTj0S2YB0

Recommended